Posts

Habari kubwa za Magazeti ya TZ leo March 8 2018 Udaku, Michezo na Hardnews

Image
Ni asubuhi nyingine tena na habari kubwa kwenye Magazeti ya Tanzania March 8 2018 kuanzia ya, Udaku, Michezo na Hardnews kujionea yote makubwa yaliyoandikwa

LEMA Ahoji Kushikiliwa kwa Mmiliki wa Shule ya Lucky Vincent Ambayo Wanafunzi Wake 35 Wamefariki na Ajali ya Basi.

Image
Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema amehoji sababu za polisi kumshikilia mmiliki wa shule ya Lucky Vincent badala ya trafiki waliokuwa barabarani siku ya ajali iliyoua watu 35. Akiomba mwongozo wa Spika kuhusu jambo hilo leo, amesema katika eneo husika kuna vizuizi vya ukaguzi vinne lakini trafiki hawakuona kuwa basi hilo lilikuwa kimezidisha watoto na hawakuwa wamefunga mikanda. Amesema badala ya trafiki hao kuchukuliwa hatua, anakamatwa mmiliki ambaye hakuwapo. Akijibu mwongozo huo, Naibu Spika, Dk Tulia Ackson amesema suala hilo halijatokea bungeni.

TETESI za Uwepo wa Al Shabab Nchini..Mwanafunzi wa Chuo cha St Joseph Akamatwa Akiwa na Bastola Yenye Risasi 13.

Image
Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Joseph,  Lazaro Mbise (23) anashikiliwa na jeshi la polisi kwa kosa la  kukutwa na bastola pamoja na risasi 13 ambayo alimwibia baba yake. Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro amesema mwanafunzi huyo alipokamatwa alikiri kuiba bastola hiyo pamoja na fedha kiasi cha Sh800, 000. “Bastola hiyo ni LUGER cz100 mtuhumiwa alikiri aliiba pamoja na risasi kutoka kwa baba yake,” amesema Sirro. Kamishna Sirro ameagiza mzazi wa mtuhumiwa kukamatwa ili afikishwe mahakamani kwa kosa la kutohifadhi bastola yake vizuri.

Askofu Gwajima kutembelewa na Maalim Seif leo

Image
Dar es Salaam.Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif,  leo saa 10 jioni atamtembelea Askofu Josephat Gwajima ofisini kwake Kanisani, Ubungo. Taarifa iliyotolewa na Kaimu Naibu Mkurugenzi wa Habari, Uenezi na Mahusiano wa CUF, Mbarara Maharagande imeeleza kuwa Maalim Seif anakwenda kumjulia hali Askofu Gwajima kumfariji na kuzungumza naye masuala mbalimbali yanayoendelea nchini. Maalim Seif amekuwepo Dar es Salaam kikazi kwa siku kadhaa sasa ambapo pia amevitembelea vyombo mbalimbali vya habari.

Adhabu ya Mwalimu Mkuu yasababisha kifo cha mwanafunzi

Image
Mwanafunzi mmoja wa shule ya msingi Matwiga wilayani Chunya mkoani Mbeya, Daudi Kaila, amefariki dunia na mwenzie baada ya kufungiwa kwa muda wa saa mbili na mwalimu wao mkuu kwenye chumba cha hazina ikiwa ni adhabu ya kosa la kutohudhuria shuleni takribani siku tano. Mwenyekiti wa Kijiji cha Matwiga, Nehemia Muga amethibitisha kutokea kwa kifo cha mtoto huyo huku walimu wa shule hiyo wakitoroka muda mfupi baada ya tukio hilo kutokea. Kwa upande wa wanafunzi waliokuwepo shuleni hapo walisema kuwa “Mwalimu akaanza kuita mwanafunzi mmoja mmoja fulani aje hapa, unaulizwa kama huna kosa unaenda kwahiyo hao wawili akawachukua mmoja alikuwa anaomba msamaha akamkatalia akawachukua wanafunzi wawili akasema mpelekeni huko baada ya kuwapeleka kwenye chumba hicho akawafungia na kufuli.” Matukio mbalimbali ya unyanyasaji wa wanafunzi Mkoani humo yamekuwa yakiendelea baada ya wiki kadhaa kupita mwanafunzi wa Mbeya day kuadhibiwa na walimu kwa kupigwa fimbo mfululizo. Nikukumbus...

Diamond baada ya Profesa Jay kuongelea bungeni milioni 400 anazodaiwa (+Video fupi)

Image
Mwimbaji wa Bongofleva Diamond Platnumz ambaye juzi aliandikwa na gazeti la NIPASHE kwamba anadaiwa shilingi milioni 400 za kodi na TRA , amechukua time yake kupost kipande cha video fupi ambacho Mbunge wa Mikumi Joseph Haule ‘ Profesa Jay ‘ amemuongelea bungeni. Kwenye video hiyo ambayo Profesa Jay amesema ‘ Juzi Msanii Diamond alikua analalamika TRA wamempelekea kodi ya Milioni 400, unaweza kujiuliza anadaiwa milioni 400 kwa kiasi gani alichoingiza? ‘ ‘ Downloads zinazofanyika mnaweza kuona Wasanii sasa hivi wanabanwa, TRA wanatamani kuvuna kutoka kwa Wasanii kitu ambacho bado hawajakipandikiza, tumekua na ule msemo kama wa zamani kwamba shamba likiwa na bangi ni lako lakini likiwa na dhahabu ni la serikali… tunataka kuchuma kitu ambacho hatujakipanda, inabidi Serikali ianze kuwekeza na kuwajenga Wasanii kutoka shule za msingi mpaka Chuo kikuu ‘ Baada ya maneno hayo ya Profesa Jay kwenye video, Diamond Platnumz ...

WAFAHAMU Wasanii Wanaoingiza Pesa Nyingi Afrika Kwa Mujibu wa Forbes

Image
Jarida la Forbes Africa la mwezi May 2017 limeandaa list ya wasanii 10 wanaoingiza pesa nyingi zaidi Africa. List hiyo ambayo inaongozwa na msanii wa Nigeria, Akon na nafasi ya pili ikichukuliwa na producer na msanii wa Afrika Kusini, Black Coffee imendaliwa kwa vigezo vya thamani ya endorsement wanazozipata, umaarufu, viwango vya show zao wanazofanya, mauzo, tuzo, watazamaji wao kwenye chaneli za YouTube, kutokea kwenye magazeti, kuwa na ushawishi mkubwa kuliko wengine, uwekezaji na uwepo wao katika mitandao ya kijamii. 1.AKON Akon anaingia kwenye list hii kutokana na mauzo ya albumu zake akribani milioni 35 zilizouzwa kila pande ya dunia, kingine kikubwa ni kwamba Akon ameshajinyakulia grammy tano huku akiwa ameingiza ngoma 45 katika chati za ya Billboard hot 100. 2. BLACK COFFEE, AFRIKA KUSINI Maarufu sana kutokana na tuzo ambazo amewahi kujishindia kama BET, wengi wanamfahamu kwa jina kamili la Nkosinathi Maphumulo , kubwa zaidi Black Coffee, ameingia kwenye...