Askofu Gwajima kutembelewa na Maalim Seif leo


Dar es Salaam.Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif,  leo saa 10 jioni atamtembelea Askofu Josephat Gwajima ofisini kwake Kanisani, Ubungo.

Taarifa iliyotolewa na Kaimu Naibu Mkurugenzi wa Habari, Uenezi na Mahusiano wa CUF, Mbarara Maharagande imeeleza kuwa Maalim Seif anakwenda kumjulia hali Askofu Gwajima kumfariji na kuzungumza naye masuala mbalimbali yanayoendelea nchini.

Maalim Seif amekuwepo Dar es Salaam kikazi kwa siku kadhaa sasa ambapo pia amevitembelea vyombo mbalimbali vya habari.

Comments