Diamond baada ya Profesa Jay kuongelea bungeni milioni 400 anazodaiwa (+Video fupi)

Mwimbaji wa Bongofleva Diamond Platnumz ambaye juzi aliandikwa na gazeti la NIPASHE kwamba anadaiwa shilingi milioni 400 za kodi na TRA, amechukua time yake kupost kipande cha video fupi ambacho Mbunge wa Mikumi Joseph HauleProfesa Jay‘ amemuongelea bungeni.
Kwenye video hiyo ambayo Profesa Jay amesema ‘Juzi Msanii Diamond alikua analalamika TRA wamempelekea kodi ya Milioni 400, unaweza kujiuliza anadaiwa milioni 400 kwa kiasi gani alichoingiza?
Downloads zinazofanyika mnaweza kuona Wasanii sasa hivi wanabanwa, TRA wanatamani kuvuna kutoka kwa Wasanii kitu ambacho bado hawajakipandikiza, tumekua na ule msemo kama wa zamani kwamba shamba likiwa na bangi ni lako lakini likiwa na dhahabu ni la serikali… tunataka kuchuma kitu ambacho hatujakipanda, inabidi Serikali ianze kuwekeza na kuwajenga Wasanii kutoka shule za msingi mpaka Chuo kikuu
Baada ya maneno hayo ya Profesa Jay kwenye video, Diamond Platnumz aliichukua video hiyo na kuandika yafuatayo >>> ‘Ndio Maana kwenye Jimbo lako sikuja kupiga kampeni bro…kwakuwa niliijua mapema thamani na umuhimu wa Uwepo wako kwenye hilo jengo
Diamond kaiweka hii na kuandika ‘Ndio maana jimboni kwako sikuja kupiga kampeni kwakua nilijua mapema umuhimu wa uwepo wako @ProfessorJayTz

Comments