TETESI za Uwepo wa Al Shabab Nchini..Mwanafunzi wa Chuo cha St Joseph Akamatwa Akiwa na Bastola Yenye Risasi 13.
Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Joseph, Lazaro Mbise (23)
anashikiliwa na jeshi la polisi kwa kosa la kukutwa na bastola pamoja
na risasi 13 ambayo alimwibia baba yake.
Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro amesema
mwanafunzi huyo alipokamatwa alikiri kuiba bastola hiyo pamoja na fedha
kiasi cha Sh800, 000.
“Bastola hiyo ni LUGER cz100 mtuhumiwa alikiri aliiba pamoja na risasi kutoka kwa baba yake,” amesema Sirro.
Kamishna Sirro ameagiza mzazi wa mtuhumiwa kukamatwa ili afikishwe mahakamani kwa kosa la kutohifadhi bastola yake vizuri.
Comments
Post a Comment