ORODHA ya Vyakula Vinavyosaidia Kulinda Afya ya Figo.
Afya ya figo ni muhimu kama ilivyo afya ya moyo, hii ni kwa sababu figo
ni moja ya kiungo ambacho husaidia kuchuja sumu mbalimbali ndani ya
mwili na baadaye kutoa taka mwili kwa njia ya haja ndogo (mkojo)
Matatizo ya figo huweza kuchangia ugumu wa upatikanaji wa haja ndogo (mkojo) au miguu na mikono kuvimba.
Pia mtu mwenye shida ya figo huwa katika hatari kubwa ya kukumbwa na matatizo ya moyo.
Ulaji unaofaa mara zote husaidia sana kulinda afya ya viungo vyote
muhimu ndani ya mwili ikiwa ni pamoja na figo na kuifanya iweze kufanya
kazi zake vizuri ndani ya mwili.
Hata hivyo, kuna baadhi ya vyakula ambavyo tunaweza kusema ni vyakula
rafiki kwa afya ya figo ndani ya mwili ni vyema ukafahamu hapa leo.
Karibu>>>
Kabeji, hii ni mboga ambayo wengi wetu tunaifahamu sana na tumekuwa
tukiitumia katika maisha yetu ya kila siku, lakini ni vyema msomaji
wangu ukatambua kwamba mboga hii nayo inauwezo mzuri wa kulinda afya ya
figo yako.
Samaki pia ni muhimu sana kwa afya ya figo, hii ni kwa sababu kitoweo
hiki kina kirutubisho kiitwacho omega 3 ambayo huwa na nafasi nzuri ya
kulinda afya ya figo, lakini pia samaki ni chanzo kizuri cha protini
ndani ya mwili.
Pamoja na hayo, mafuta ya mzaituni nayo ni mazuri sana kwa kuboresha afya ya figo na kuikinga dhidi ya magonjwa mbalimbali.
Mafuta haya ya mzaituni ndani yake yana virutubisho mbalimbali kama
'oleic acid', anti-inflammatory fatty acids ambavyo vyote kwa pamoja
hutetea afya ya figo ndani ya mwili, halikadhalika mafuta haya ni mazuri
pia kwa afya ya moyo.
Comments
Post a Comment