Mourinho awakebehi mashabiki wa Arsenal
Meneja wa Klabu ya Manchester
United, Jose Mourinho ameonekana kuwa mwenye furaha baada ya kuwaona
mashabiki wa Arsenal wakishangilia baada ya kufanikiwa kuichapa United
2-0 jana usiku .
Mourinho amesema ni mara yake ya kwanza kuwaona mashabiki hao
wakionesha sura za furaha katika maisha yake tena kwa ushindi huo wa
kwanza wa Arsene Wenger katika mechi 16 za ushindani dhidi ya timu
iliyokuwa chini ya Mourinho.“Niliondoka Highbury na walikuwa wanalia, nikaondoka Emirates na walikuwa wanalia,Hatimaye leo wanaweza kuimba, wanarusha skafu hewani,Ni jambo zuri kwao.” Alisema Mourinho huku akiendelea kuzungumzia rekodi ya timu ya Arsenal na timu alizowahi kuzinoa.
“Ni mara ya kwanza kwamba naondoka na wamefurahi. Awali, walikuwa wakiondoka wanatembea wameinamisha vichwa barabarani,Mashabiki wa Arsenal wana furaha na nina furaha kwa sababu ya hilo.”Alisema Mourinho mapema kwenye mahojiano yake baada ya Mechi kumalizika jana usiku.
Mechi pekee ambayo Arsenal waliwahi kushinda dhidi ya Mourinho wakiwa na Wenger ilikuwa mwaka 2015 wakati wa mechi ya Ngao ya Jamii Mourinho alipokuwa Chelsea.
Klabu za wawili hao zilikutana kwa mara ya kwanza Desemba 2004 – Gunners walipokuwa bado wanatumia uwanja wa Highbury – mechi iliyoisha kwa sare ya 2-2 .
Comments
Post a Comment