Mbunge Australia anyonyesha mtoto bungeni
Senator kutoka jimbo la Queensland nchini Australia, Larissa Waters, ameweka historia bungeni hapo alipomleta kazini na kumnyonyesha mwanaye wa miezi miwili ikiwa ni mara ya kwanza na hivyo kutengeneza historia hiyo nchini humo.
Larissa Waters amerejea kazini baada ya likizo ya uzazi na mwanaye huyo, huku akiwa tayari kutumia uhuru wake wa sheria mpya inayowaruhusu wazazi ambao ni senator,nchini Australia kuja na vichanga vyao na vilevile kuwanyonyesha punde wanapopatwa na njaa.
Comments
Post a Comment