Fahamu kuhusu ujio wa SportPesa Tanzania



Waswahili husema Leo ndio leo na asie na mwana aeleke jiwe. Siku muhimu kabisa iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wana familia wa soka nchini hatimae imewadia.
Kampuni mpya ya kubashiri michezo ya Sport pesa, inatarajia kuzinduliwa nchini rasmi leo.

Kampuni hii inazinduliwa rasmi kwa mara ya kwanza nchini,ikiwa ni kampuni maarufu katika ukanda huu wa Africa Mashariki na kati na yenye makao makuu yake nchini Kenya na watu wakijishindia mabilioni ya fedha.
Hali hiyo imefanya watu wengi wanaopenda michezo hiyo ya kubashiri kutamani siku moja SportPesa ianze kazi hapa nyumbani.
“Nilikuwa nasikia tu Sportpesa watu wanashinda mamilioni kama  yule wa juzi nilimsikia Radioni watu wakimzungumzia  hata mitandaoni nilikuwa  naona picha zake nawafuatilia sana SportPesa, nadhani ni muda mzuri na mimi kujaribu bahati yangu”  alisema mdau mmoja wa michezo ya kubashiri.
Uwepo wa kampuni hii katika michezo nchini Kenya imesaidia kwa kiasi kikubwa kurejesha ari na hamasa katika michezo nchini humo baada tu ya kuidhamini ligi hiyo. Ikumbukwe Sportpesa imewadhamini  klabu kongwe ya Kenya Gor Mahia na AFC Leopards na kusababisha kurudisha ushindani wa ligi ya Kenya.
Sport pesa wameendeleza kutanua mipaka kwa kudhamini klabu ya ligi kuu nchini Uingrereza, klabu ya Hull City.
Ujio wa Sportpesa nchini utazinufaisha vilabu vya soka hapa nyumbani na kuweza kupata  ligi yenye Msisimko  kwani tayari wanatarajia kuidhamini klabu kongwe ya Yanga Sc.
Karibu Sport pesa, hakika utakuwa mkombozi wa vilabu vyetu hapa nchini, ili tuweze kupata ligi yenye ubora na ushindani karibu sana Mgeni.
BY HAMZA FUMO NA GODFREY MGALLAH

Comments