Magonjwa Haya, Huathiri Nguvu za Kiume na Kuharibu Kizazi kwa Wote, Wake na Waume.
KUNA magonjwa mengi tofauti ya zinaa, lakini yale ambayo yameenea sana
ni kisonono, kaswende, klamdia, kankroidi, utando mweupe, Virusi Vya
Ukimwi na Ukimwi. Magonjwa mengi ya zinaa ni kwamba dalili zake
hazionekani kwa urahisi na kama yasipotibiwa kikamilifu yanaweza kuleta
madhara makubwa. Tuchambue kwa ufupi magonjwa hayo:
Kisonono:
Huchukua muda wa siku moja hadi 14 tangu kuambukizwa mpaka kuonyesha
dalili za kuumwa. Kwa wanawake dalili za kisonono ni maumivu chini ya
tumbo ambayo yanaweza kuambatana na homa na kutokwa uchafu ukeni. Wapo
wanawake wengine ambao hawaoni dalili zozote. Athari yake kwa mwanamke
ni kuziba mirija ya kupitisha mayai na mimba kutunga nje ya mfuko wa
uzazi, na vilevile ugumba.
Kwa mtoto aliye tumboni mwa mama mjamzito kisonono cha mama yake
kinaweza kusababisha upofu. Kwa mwanaume athari yake ni kuziba mirija ya
kupitisha mkojo. Kwa wanaume dalili ni kutokwa na usaha uumeni na
kupata maumivu wakati wa kukojoa.
Kaswende:
Dalili ya kaswende kwa mwanamke ni vidonda sehemu za siri hasa kwenye
mashavu ya uke na sehemu ya njia ya haja kubwa, pamoja na sundosundo
sehemu ya siri. Kwa mwanaume dalili ni vidonda. Mara nyingi kimoja
kwenye kichwa cha uume, kwenye kishina cha uume na kuzunguka njia ya
haja kubwa.
Pia mwanaume anaweza kupata sundosundo sehemu za siri. Ugonjwa huu
husababisha matatizo ya moyo na kuharibu ubongo na kuzaa watoto
walemavu.
Klamdia:
Dalili yake kwa mwanamke mara nyingi siyo rahisi kuonekana. Kwa mwanaume
dalili ni kupata maumivu wakati wa kukojoa, na kukojoa mara kwa mara.
Athari kwa mwanamke ni kuziba kwa mirija ya kupitisha mayai na mimba
kutunga nje ya mfuko wa uzazi. Mimba hizi kuhatarisha maisha ya mama na
kuleta ugumba vinaweza kutokea.
UtasaKankroidi:
Dalili yake ni vidonda sehemu za siri vinavyokuwa na maumivu makali,
maumivu wakati mkojo unapopita kwenye vidonda na kuvimba tezi sehemu za
siri. Tezi huweza kupasuka na kutoa uchafu na maumivu makali. Utando
mweupe: Dalili kwa mwanamke ni kutokwa na uchafu ukeni (kama maziwa
yaliyoganda), kuwashwa na kuwa na michubuko sehemu za siri. Kwa mwanaume
ni kuwashwa sehemu za siri na kusikia maumivu wakati wa kukojoa. Athari
ni maumivu wakati wa kujamiiana.
Virusi Vya Ukimwi:
Katika hatua ya mwanzo baada ya kuambukizwa hakuna dalili maalum. Hatua
hii inaweza kuchukua mpaka miaka kumi. Lakini mara mtu anapoanza kuugua
Ukimwi dalili zinakuwa nyingi. Pamoja na kupungua kinga ya mwili,
kupungua uzito na kuumwa mara kwa mara.
Comments
Post a Comment