HALI ya Sukari Nchini Kizingumkuti..Bei Yapaa Hadi 2800 kwa Kilo Moja
LICHA ya kuwepo kwa wafanyabiashara wachache wa sukari wasio waaminifu
mkoani Mwanza kupandisha bei ya bidhaa hiyo kwa asilimia 22 kutoka
Shilingi 2,300 hadi 2,800 kwa kilo moja, uzalishaji wa sukari umepanda
hadi kufikia tani 326,000 kwa mwaka 2016/2017.
Kupanda kwa kiwango hicho cha uzalishaji sukari nchini kumebainishwa na
Mwenyekiti wa mfuko wa maendeleo wa sekta ya sukari Tanzania (SIDTF),
Deo Lyatto, wakati wa kikao cha wataalamu wa sukari cha kujadili
changamoto zinazoikabili sekta hiyo.
Kwa upande wa wazalishaji wa sukari na wakulima wa miwa nchini na nje
wameishauri serikali kutoa ushirikiano wa kutosha katika sekta hiyo ili
kujenga uchumi na kuwezesha adhima ya serikali kuwa na nchi ya viwanda.
Naye Mkurungenzi wa bodi ya sukari nchini, Henry Semwanza, alisema huu
ni muda muafaka kwa wazalishaji wa sukari kuongeza jitihada katika
kuzalisha bidhaa zenye ubora na kuuza kwa bei ya chini ambayo wanachi wa
hali ya chini waweze kumudu bei hiyo.
Comments
Post a Comment