BREAKING NEWS: Tetemeko jingine latokea Bukoba

Reporter wa AyoTV na millardayo.com ameripoti kutokea mtaa wa Rwamishenye manispaa ya Bukoba kwamba limetokea tetemeko. Amesema tetemeko hilo ambalo limetokea mida ya saa saba na nusu usiku huu wa kuamkia April 30, lilidumu kwa sekunde zisizozidi 15.
Mpaka sasa anazunguka kwenye mitaa mbalimbali na anachoshuhudia ni Watu mbalimbali waliotoka nje ya nyumba zao kuhofia tetemeko jingine. Hakuna madhara yoyote yaliyoripotiwa mpaka sasa lakini AyoTV na millardayo.com zinaendelea kufatilia kwa ukaribu.
Hakikisha umejiunga na APP ya ‘millardayo’ pia Twitter FB na Instagram zenye jina la ‘millardayo’ ili kila breaking news ikufikie kwa wakati.

Comments