Viongozi wa timu ya Simba SC watoa neno kuhusu nyasi zao bandia kupigwa mnada

Kampuni ya udalali ya Majembe Auction Mart inataka kupiga mnada nyasi bandia za klabu ya Simba SC pamoja na magoli yake, sababu kubwa ni uongozi (wamiliki) kushindwa kuzilipia kodi.

Sababu hasa za kupigwa mnanda kwa nyasi pamoja na magoli yake ni timu ya Simba kushindwa kulipa kodi ya Shilingi milioni 80 wanazodaiwa na TRA.
Mnada utafanyika siku ya leo Alhamisi 30/03/2017.
Eneo:Nyuma ya “The Waterfront Sunset Restaurant and Beach Bar”, barabara ya Yatch Club, Masaki, ofisi mnada utakaofanyika zinaitwa LW9.

Makamu wa Rais wa Simba, Geoffrey Nyange ‘Kaburu’ amesema leo kwamba wana taarifa za mpango wa kupigwa mnada nyasi hizo na wapo kwenye mchakato wa kuzikomboa.
“Ni kweli kwa kawaida Bandarini kuna utaratibu, mzigo unapofika lazima ulipiwe utoke, ikishindikana hivyo unapigwa mnada. Kwa hiyo lazima tujitahidi tuzikomboe,”alisema.
Nae mwenyekiti wa Kamati ya Maendeleo ya Ujenzi wa Uwanja Bunju Complex wa klabu hiyo, Zacharia Hans Poppe amesema kwamba anashangaa kusikizia nyasi hizo bado hazijalipiwa, wakati fedha zilikwishapatikana.
“Unaponiambia hivyo ninashangaa, kwa sababu tulikwishafanya mpango fedha zikapatikana za kulipia hizo nyasi, sasa kuambiwa hazijalipiwa hadi sasa sijui ni kwa nini,”alisema Hans Poppe na kuongeza; “Ngoja niwasiliane na wenzangu, mimi nipo Kenya kwa sasa,”alisema.

Comments