UTAFITI: Wanasayansi wagundua matatizo ya kiafya yanayotokana na mbio za Marathon


Wakati Dunia ikiamini kuwa kufanya mazoezi hasa ya kukimbia kunajenga afya ya mwili utafiti unaonesha kuwa mbio za Marathon zinaweza kuathiri afya ya mtu ambapo wanasayansi wametoa onyo baada ya utafiti kugundua kuwa 80% ya wanaokimbia mbio hizo hupata matatizo ya figo kwa sababu ya upungufu wa maji mwilini, ‘dehydration’.
Utafiti huo umechapishwa kwenye Jarida la American Journal of Kidney Diseases, katika kipindi ambacho maelfu ya watu wakijiandaa kwa ajili ya mbio za London Marathon mwezi ujao.

Jopo la watafiti likiongozwa na Professor Chirag Parikh, wa Yale University, Marekani, walilifanyia utafiti kundi dogo la washiriki wa Hartford Marathon mwaka 2015 wakichukua sampuli za damu na mkojo kabla na baada ya mbio ambapo baada ya uchunguzi waligundua 82% ya wakimbiaji waliotafitiwa walionesha Stage 1 Acute Kidney Injury (AKI) muda mfupi baada ya mbio. AKI ni hali ya figo kushindwa kuchuja uchafu kutoka kwenye damu.
“Figo zilionesha mkazo wa kifizikia kwa wakimbiaji wa marathon kama kwamba zimejeruhiwa, katika namna inayofanana na kinachotokea kwa wagonjwa wa Hospitali wakati figo zinapoathiriwa na dawa na matatizo ya upasuaji.” – Professor Chirag Parikh.

Watafiti wanaeleza kuwa sababu za kuharibika figo kutokana na mbio za marathon zinaweza kuongezeka kutokana na hali ya joto la mwili, upungufu wa maji mwilini, au kushuka kiwango cha usambazaji wa damu kwenye figo ambao hutokea wakati wa marathon.
Wakati tatizo la kuumia figo likiweza kutatuliwa ndani ya siku mbili za kukimbia marathon, watafiti wanasema utafiti bado unaibua maswali kuhusu athari kuweza kujirudia zaidi na zaidi, hasa kwenye majira ya joto….“Tunahitaji kuchunguza hili zaidi.” – Prof. Parikh

Comments